UINGEREZA IMEANZA KUBANA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

Kwa waziri mkuu wa Uingereza tofauti baina ya mema na mabaya ipo wazi kabisa mithili ya usiku na mchana. Mashirika ya ujasusi yanapambana na magaidi na anaetoa habari zozote juu ya kazi za mashirika hayo ni adui.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron akizungumza na waandishi wa habari mjini Brussels Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron akizungumza na waandishi wa habari mjini Brussels
Mwandishi wetu Regina Menning anasema katika taarifa yake kwamba Uingereza inaelekea katika mkondo wa kuubana uhuru wa vyombo vya habari kwa kisingizio cha kuulinda usalama wa taifa.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron aliufafanua msimamo huo kandoni mwa mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya uliofanyika mjini Brussels hivi karibuni. Alipozumzia juu ya adui, Waziri Mkuu Cameron alikuwa na maana ya Edward Snowden wakala wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani ka NSA aliefichua siri za shirika hilo. Kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Cameron vyombo vya habari, kama gazeti la "Guardian "pia ni adui wa harakati za kupambana na ugaidi .
Gazeti la Uingereza la The Guardian linadaiwa kuwa adui wa harakati za kupambana na ugaidi
Add caption
Gazeti la Uingereza la "The Guardian" linadaiwa kuwa adui wa harakati za kupambana na ugaidi
Mwandishi wa gazeti hilo Glenn Greenwald alizichapisha habari za kwanza za siri alizopewa na aliekuwa mfanyakazi wa shirika la ujasusi la Marekani la NSA, Edward Snowden. Waziri Mkuu wa Uingereza ametoa vitisho dhidi ya gazeti la "Guardian" Na siyo yeye peke yake.
Kwa muda wa wiki kadhaa sasa vyombo vya habari muhimu nchini Ungereza vimekuwa vinalisakama gazeti la Guardian. Vyombo hiyvo vinesema katika tahariri kali kwamba kwa kukubali kuzichapisha siri zilizofichuliwa na Edward Snowden, gazeti hilo limewasaida maadui wa Uingereza. Kiongozi wa maripota wasiojali mipaka tawi la Ujerumani Michael Rediske amesema vitisho kama hivyo ni jambo lisilowezekana nchini Ujerumani.Amekumbusha juu ya mzigo wa historia unaobebwa na wajerumani.
Nchini Ujerumani watu wanakumbuka yaliyotokea wakati wa utawala wa mafashisti.Dhana kama maslahi ya kitaifa au siri za nchi zilitumika kama sababu. Katika baadhi ya nchi, miongoni mwao ,Uingereza vitabu vya sheria vinatumiwa kuimarisha ulinzi wa siri za nchi."
Mkuu huyo wa waandishi wa tawi la Ujerumani la waandishi wa habari wasiojali mipaka bwana Rediske amesema vyombo vya habari nchini Ujerumani vina makucha ya kuwaewzesha kujitetea.Ametoa mfano wa alieyekuwa Rais wa Ujerumani, Christian Wulff aliejaribu kumtisha mhariri mkuu wa gazeti la "Bild.
Rais huyo wa zamani alimpigia simu mhariri huyo ili kujaribu kuzuia kuchapishwa kwa taarifa juu ya mkopo uliokuwa na utata aliopewa bwana Wulff. Mkasa huo ulitifua tufani iliyomng'oa madarakani Rais huyo. Lakini serikali ya Uingereza inavishinikiza vyombo vya habari kwa kisingizio cha usalama wa taifa. Hata hivyo mwakilishi wa waandishi habari wasiojali mipaka bwana Rediske amesema inapasa kutilia maanani kwamba magaidi waliwahi kufanya mashambulio mabaya katika treni ya chini ya ardhi nchini Uingereza.

0 comments:

DUNIA YACHUKUA HATUA KUBWA KUPAMBANA NA VIFO VYA WATOTO

Dunia imepiga hatua kubwa isio na kifani katika kupunguza idadi ya vifo vya watoto katika kipindi cha muongo mmoja uliopita huku Niger ikitajwa kuwa inaongoza kundi lililopiga hatua kubwa zaidi duniani tokea mwaka 1990.
Watoto wa Kiafrika Watoto wa Kiafrika.
.Katika ripoti iliyotolewa leo hii Shirika la kuawaokoa watoto Save the Children limeonya kwamba hakuna nafasi ya kuregeza kamba.
Ripoti ya shirika hilo iliopewa kichwa cha habari "Maisha Hatarini" imeangalia jinsi nchi 75 zinavyoshughulikia malengo ya kupambana na vifo vya watoto yaliowekwa na Umoja wa Mataifa hapo mwaka 2000 katika kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Milenia Malengo hayo ni pamoja na kupunguza kwa theluthi mbili vifo vya watoto ifikapo mwaka 2015.
Ripoti hiyo inasema idadi ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wanaokufa kutokana na sababu zinazozuilika kama vile utapia mlo au ukosefu wa madawa kila mwaka, takriban imepunguwa kwa nusu kutoka milioni 12 hapo mwaka 1990 hadi kufikia milioni 6.6 hapo mwaka 2012.
Nchi zilizotia fora
Watoto wa Msumbiji. Watoto wa Msumbiji.
Mbali na Niger miongoni mwa mataifa 10 ambayo yamepiga hatua kubwa katika kupambana na vifo vya watoto ni Liberia,Rwanda, Indonesia, Madagascar, India, China,Misri,Tanzania na Msumbiji.Kwa mujibu wa repoti hiyo ya shirika lisilo la kiserikali upande ambapo bado tatizo hilo ni kubwa, nchi ambazo hazikupiga hatua kubwa ni pamoja na Haiti, Papua New Guinea na Equatorial Guinea.
Hata hivyo kiwango cha vifo vya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano ambavyo sio vya lazima bado ni kikubwa nchini Niger. Lakini kimepunguzwa sana kwa theluthi mbili kutoka 1,000 hadi 326 hapo mwaka 1990 na kutoka 1,000 hadi 114 hapo mwaka 2012.
Sehemu kubwa ya mafanikio yake imetokana na yale makundi yenye kipato.Hata hivyo Nigeri ikiwa ni mojawapo ya nchi maskini kabisa duniani inatekeleza mipango ya lishe na kutowa huduma bure za matibabu kwa wanawake wajawazito na watoto.
Dunia iko nje ya lengo
Lakini kwa jumla dunia iko nje ya lengo lililowekwa ambapo kiwango kikubwa cha vifo vya watoto kinazidi kujitokeza miongoni mwa nchi maskini duniani.
Kwa mfano Afrika magharibi na Afrika Kati imekuwa na asilimia 17 ya vifo vya watoto hapo mwaka 1990 na kuongezeka hadi asilimia 30 hapo mwaka 2013,vingi ya vifo hivyo vikitokea katika nchi zilizokumbwa na mizozo.
Utapia mlo bado ni tatizo Afrika. Utapia mlo bado ni tatizo Afrika.
Patrick Watt mkurugenzi wa kampeni wa Shirika la Save the Children amesema maisha ya watoto milioni nne pia yangeliweza kuokolewa katika kipindi cha muongo mmoja uliopita ingelikuwa matumizi yangelikuwa sawa katika kupambana na vifo vya watoto miongoni mwa makundi yenye kipato.
Watt amekaririwa akisema wanapiga hatua za kihistoria katika vita dhidi ya vifo vya watoto lakini mafanikio hayo yasio kifani pia mara nyingi hufunika watoto wa kimaskini wanaoachwa nyuma ambapo katika kesi nyengine hali zao zinakuwa mbaya kupindukia.
Shirika hilo limezihimiza serikali kutekeleza mipango ya afya ya taifa ambayo inamfikia kila mtoto,wakiwemo watoto wachanga ambao ndio kwanza wamezaliwa kwa lengo la kuifanya mipango hiyo iwe inapatikana kikamilifu ifikapo mwaka 2030 na kupunguza utapia mlo ili kwamba kila mtoto awe anapata lishe wanayohitaji ili kuendelea kuishi na kunawiri.
Mwandishi: Mohamed Dahman/AFP/dpa
Mhariri: Moahammed Abdul-Rahman

0 comments:

VIJANA WA NAAMBUKIZANA IKIMWAI KWA KUTIKUA NA ELIMU

Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni - UNESCO limesema zaidi vijana 50 waliofikia umri wa kubalehe katika nchi za Kusini na Afrika Mashariki wanaambukizwa virusi vya ukimwi kila siku
Hali hiyo inatokana na wao kukosa elimu ya uzazi. Kutokana na hatua hiyo, UNESCO imeanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kutoa msukumo kwa nchi kuhaksha kwamba mitaala ya elimu inakidhi viwango vya elimu ya uzazi itayowasaidia vijana hao kufanya maamuzi pindi watapojihusisha na masula ya mapenzi. Hayo yamebainika nchini Tanzania wakati shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilipozindua ripoti mpya kuhusu vijana na balehe yenye kauli mbiu isemayo “Vijana wa Leo-Muda wa kuchukua hatua sasa”
Katika utafiti wake uliofanya katika mataifa 21, yaliyoko Kusini na Mashariki mwa Afrika, UNESCO ilibaini kasoro kadhaa ikiwemo kukosekana kwa mitaala maalumu inayoangazia afya za uzazi kwa vijana. Hali hiyo ndiyo iliyotajwa kuwa imechangia kwa kiwango kikubwa kwa vijana hao kutokuwa na maamuzi sahahi pindi wanapoanza kujishughulisha na masuala ya kipamapenzi.
Utafiti huo pia ambao umewajumuisha wataalamu kutoka taasisi za umma, mashirika ya kiraia nay ale ya Umoja wa Matifa ikiwemo UNICEF na WHO, inanoyesha kuwa, kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi kwa makundi ya vijana kumesabisha mamia ya wanafunzi wa kike kuacha shule kila siku kutokana na kupata mimba.
Ukosefu wa elimu ya uzazi pia kumesababisha wanafunzi wa kike kuwacha shule kila siku kutokana na uja uzito Ukosefu wa elimu ya uzazi pia kumesababisha wanafunzi wa kike kuwacha shule kila siku kutokana na uja uzito
Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Mtaalamu wa UNESCO Mathias Faustini alisema kkuwa pamoja na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo la mimba shulenni na upunguzwaji maambukizi ya virusi vya HIV kwa vijana, lakini ozeefu umeonyesha kuwa juhudi hizo zimekosa mikakati ya kisanyansi.
Hata hivyo ili kukabiliana na hali hiyo UNESCO kushirikiana na nchi zilizoko katika Jumuiya ya Maendeleo Kusin mwa Afrika(Sadc) na zile zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kuteleza mpango wa pamoja ambao uhakikisha elimu kwa vijana inaboreshwa.
Tayari mkakati wa awali umeandaliwa ambao utajadiliwa katika kikao kinachotazamiwa kufanyika mwanzoni mwezi Disemba nchini Afrika Kusin, kikiwa husisha mawaziri Wizara za Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Elimu na Masuala ya ufundi kutoka katika nchi zote wanachama.
Baadhi ya makundi ya wanafunzi pamoja na watetezi wa maslahi ya vijana yameanza kupaza sauti yakitoa mwito kwa mamlaka za kidola kuanz akumulika utendaji wake wa mambo.
Kuanzishwa kwa mkakati huo wa upitiaji mitaala ya elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kunatajwa na wengi pengine kunaweza kusaidia kupunguza matatizo yanayowaandama vijana wananza kubalehe.
Mwandishi: George Njogopa
Mhariri: Josephat Charo

0 comments:

AJARI YYA TRENI NA BASI YAWAUWA WATU 12, NAIROBI KENYA

Kiasi ya watu 12 wameuawa baada ya treni la abiria kuligonga basi lililokuwa likivuka reli jijini Nairobi, Kenya. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema watu wengine wamejeruhiwa kufuatia ajali hiyo mbaya
Mabaki ya basi la abiria lililogongwa na treni jijini Nairobi Mabaki ya basi la abiria lililogongwa na treni jijini Nairobi
Ajali za barabarani zinazosababisha idadi kubwa ya vifo hutokea kila mara nchini Kenya. Kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabara na mabasi yanayojaa abiria kupinduka, kila mara huendeshwa kwa mwendo wa kasi na kuyapita magari mengine ili kupata faida ya haraka.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, gari hilo lilikokotwa kwa takribani mita 500 kutoka eneo la ajali. Mkuu wa polisi jijini Nairobi Benson Kibui amesema basi hilo la abiria lilivuka reli wakati treni hilo lilipofika kwa mwendo wa kasi. Ajali hiyo ilitokea wakati wakaazi wengi wa jiji walipokuwa wamejaa barabarani wakielekea makazini saa za asubuhi.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri:Josephat Charo

0 comments:

OBAMA ALIJUA NINI HASA?

Bado mpaka sasa Rais Barack Obama na Shirika la Ujasusi (NSA) wanatafuta la kusema baada ya kudhihirika kwamba simu ya mkononi ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ilikuwa ikitegwa na maafisa wa ujasusi wa Marekani.
Picha inayoashiria unasaji wa simu za Ujerumani uliofanywa na Marekani. Picha inayoashiria unasaji wa simu za Ujerumani uliofanywa na Marekani.
Gazeti la kila Jumapili la "Bild am Sonntag" linalosomwa na watu wengi nchini Ujerumani jana (tarehe 27 Oktoba) liliripoti kwamba Rais Obama alijua kwamba simu ya mkokoni ya Kansela Merkel ilikuwa inasikilizwa na NSA tokea mwaka 2010. Shirika hilo limeyakanusha madai hayo, lakini bado pana hitilafu nyingi.
Ikulu ya Marekani imenyamaza kimya na NSA inasubiri. Msemaji wa Idara ya Ujasusi ya Marekani ameeleza kuwa ripoti ya "Bild am Sonntag" siyo sahihi. Mkuu wa NSA, Keith Alexander, hakumpa taarifa Rais Obama binafsi juu ya shughuli za kusikilizwa kwa simu ya Kansela wa Ujerumani na NSA. Pana madai kwamba Mkurugenzi wa NSA na Rais Obama asilani hawakuzungumzia juu ya shughuli za upelelezi zilizomhusu Kansela Markel.
Jambo moja linaweza kuwa wazi kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la New York Times , kwamba simu ya mkononi ya Kansela Merkel ilianza kusikilizwa na majasusi wa Marekani miaka 10 iliyopita au hata kabla ya hapo. Wakati huo Merkel bado alikuwa mwenyekiti tu wa chama cha CDU.
Aliyekuwa wakala mwaminifu wa NSA kwa muda wa miaka 18, Thomas Drake, ni mtu anayepaswa kuyajua ya jioni na ya asubuhi katika shirika hilo. Amesema hakushangazwa ni kilichotokea.
Kumbukumbu za Statsi
Picha hii ya tarehe 2 Septemba 2009 inamuonesha Rais Barack Obama akiwa na Kansela Angela Merkel kwenye mkutano wa kilele wa G20 jijini London. Picha hii ya tarehe 2 Septemba 2009 inamuonesha Rais Barack Obama akiwa na Kansela Angela Merkel kwenye mkutano wa kilele wa G20 jijini London.
Kutokana na kukasirishwa juu ya kupelelezwa kwa simu za wananchi wa Marekani , Drake angelikuwa mtoboa siri siku nyingi kabla ya Edward Snowden.
Ameeleza kuwa alikuwa anatarajia kuyasikia mambo mengine yakifichuliwa kutokana na kile anachokijua kutokea ndani ya shirika la NSA. Yaliyotokea pia yanamkumbusha enzi za zamani.
"Hebu kumbuka enzi za ufashisti nchini Ujerunmani. Hebu kumbuka enzi za upelelezi wa shirika la ujasusi la Stasi katika Ujerumani Mashariki. Yaliyofanyika kwa Angela Merkel yamemgusa sana yeye binafsi kukumbuka mashambulizi ya nchini Marekani, kwa sababu wateka nyara walikuwapo nchini Ujerumani, waliishi Ujerumani na walikwenda Marekani kutokea Ujerumani. Na kwa hivyo serikali ya Marekani na shirika la NSA kwa pamoja waliamua kuwa Ujerumani inapaswa kuwa kituo kikuu cha kupelelezwa barani Ulaya."
Wakala huyo wa zamani wa shirika la NSA ameeleza kuwa yanayoibuka sasa na kutokea hadharani hayasemeki.
Thomas Drake, ambaye alifanya upelelezi dhidi ya Ujerumani ya Mashariki ya zamani, amesema kilichotokea "kinamkumbusha enzi za Statsi na pia yanamkumbusha enzi za mafashisti nchini Ujerumani."
Mwandshi wa habari aliyefichua kashfa ya Watergate, Bob Woodward, pia amezikosoa shughuli za shirika la NSA.
Mwandishi: Antje Passenheim
Tafsiri: Abdu Mtullya
Mhariri: Josephat Charo

0 comments:

BRAHIMI AKUTANA NA ASSAD MJINI DAMASCUS

Rais wa Syria, Bashar al Assad, amesisitiza ni watu wa nchi hiyo tu watakaoamua hatima ya mkutano wa kimataifa wa kutafuta amani Syria ujulikanao kama Geneva II, alipokutana na mjumbe wa amani Lakhdar Brahimi
Rais huyo wa Syria amerudia msimamo wake kuwa, ili amani irejee Syria basi nchi za kigeni sharti zisitishe msaada kwa waasi wanaotaka kumng'oa madarakani. Assad amesema ni watu wa Syria walio na haki ya kuamua hatima ya siku za usoni ya taifa lao na suluhisho au makubaliano yoyote lazima yakubalike na raia wake na yawe ya manufaa kwao.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na jumuiya ya nchi za kiarabu kwa mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi, amekutana na Assad kama sehemu ya ziara yake katika kanda hiyo inayolenga kutafuta uungwaji mkono wa kuandaliwa kwa mkutano wa kimataifa unaoandaliwa na Urusi na Marekani kwa ajili ya Syria unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Geneva.
Katika mkutano huo wa leo, Assad ameonya dhidi ya muingilio wowote kutoka nje katika mchakato wa kutafuta suluhisho la mzozo wa Syria ambao umesababisha vifo vya takriban watu 115,000 katika kipindi cha miezi 31 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuongeza kuwa lazima msaada kwa magaidi; neno ambalo utawala wake unalitumia kuashiria waasi, kukoma kama hatua muhimu ya kuafikia suluhu.
Visa vya ugonjwa wa Polio vimethibitishwa katika maeneo kadhaa nchini Syria Visa vya ugonjwa wa Polio vimethibitishwa katika maeneo kadhaa nchini Syria
Kituo cha televisheni cha serikali Syria pia kimeripoti kuwa Brahimi alikubaliana na Assad kuwa wasyria wenyewe ndiyo wanastahili kutafuta suluhisho la vita vinavyowazonga vilivyoiharibu nchi yao. Katika mkutano huo wa kwanza kati ya Brahimi na Assad tangu Desemba mwaka jana, mjumbe huyo maalumu wa umoja wa Mataifa amesema mkutano wa Geneva unanuia kuhakikisha Wasyria wanapata ufumbuzi wa mzozo huo haraka iwezekanavyo.
Huku hayo yakijiri, kiasi ya raia 800 ambao wengi wao ni wanawake, watoto na wazee waliokuwa wamekwama katika mji wa Moadamiyet al Sham uliokuwa chini ya mashambulizi makali wamehamishwa. Hayo ni kulingana na wanaharakati wa eneo hilo la kusini mwa mji mkuu Damascus.
Raia hao waliokolewa kutoka mji huo uliokuwa ukishikiliwa na waasi kufuatia usimamizi wa shirika la msalaba mwekundu ukishirikiana na pande zote zinazozozana. Picha za video za televisheni zinaonyesha watu hao wakihamishwa wakiwa wamebeba mali zao kidogo na kuondoka kutoka mji huo wakisaidiwa na maafisa wa msalaba mwekundu.
Mji huo wa Moademiyet al Sham umekumbwa na mapigano makali kwa karibu mwaka mmoja. Makundi ya kutetea haki za binadamu yameripoti utapia mlo hasa miongoni mwa watoto katika mji huo kutokana na kukatizwa kwa njia za kupitisha misaada ya kibinadaamu. Kulingana na wanaharakati, kiasi ya raia wengine 6,000 wamesalia katika eneo hilo. Waliohamishwa sasa watapelekwa katika kambi za wakimbizi viungani wma Damascus, kujiunga na mamilioni ya wasyria wengine waliobaki kuwa wakimbizi nchini mwao.
Mwandishi:Caro Robi/afp/ap
Mhariri: Josephat Charo

0 comments:

Sleeping less than 7 hours each night reduces your life expectancy.

Sleeping less than 7 hours each night reduces your life expectancy.

0 comments:

MARUBANI WATOSHA TWIGA WATUMIA HATI ZA KIDPROMASIA


Moshi na Dodoma. Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, imeelezwa kuwa marubani wa ndege ya kijeshi ya Qatar, walitumika katika kutorosha twiga wanne kwenda Uarabuni na kwamba washtakiwa walikuwa na hati za kusafiria zenye hadhi ya kidiplomasia.
Shahidi wa 13, Prisca Sabugo ambaye ni Ofisa Uhamiaji, aliiambia mahakama juzi kuwa hati hizo hazikugongwa mihuri wala kupewa viza.
Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobelo, shahidi huyo alidai kuwa ndege hiyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) Novemba 24 mwaka 2011.
“Baada ya hiyo ndege ya jeshi kutua, alikuja wakala wao kutoka Kampuni ya Equity Aviation akaniletea Diplomatic Passport zao na akaniambia wamekuja kwa shughuli za utalii kwa siku tatu,” alisema.
Huku akiongozwa na mawakili wa Serikali, Evetha Mushi na Joseph Maugo, shahidi huyo alidai kuwa marubani na wafanyakazi wa ndege huwa hawapitii utaratibu wa kawaida wa kujaza fomu na kupewa viza. Alisema, tangu wageni hao waingie nchini kama watalii, hawakuwahi kuhojiwa na chombo chochote kuhusu kutogongwa mihuri kwenye hati zao.
Shahidi wa 12, Oscar Jullius ambaye ni Ofisa Wanyamapori, alidai kuwa vibali vilivyotumika kukamata wanyama hao vilikuwa vya kampuni mbili ambazo ni Ham Market na Luega Birds Traders.
Kwa mujibu wa shahidi huyo, vibali hivyo vilikuwa vya kumiliki nyara na si vya kukamata wanyamapori hai na kwamba yeye ndiye aliyeandika ripoti ya thamani ya wanyama hao.
Alisema thamani ya wanyama wote waliotoroshwa ilikuwa ni Sh170.5 milioni na kwamba twiga hao wanne kila mmoja alikuwa na thamani ya Dola 10,000 za Marekani sawa Sh60 milioni za Tanzania.
Alipoulizwa na mmoja wa mawakili wanaowatetea washtakiwa, Edmund Ngemela, kama vibali walivyokuwa navyo vilikuwa halali, alikiri kuwa vilikuwa halali na vilikuwa ni vya kumiliki nyara.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea Novemba 29 mwaka huu.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni pamoja na raia wa Pakistan, Kamran Ahmed, Hawa Mang’unyuka, Martin Kimath na Michael Mrutu ambao wote wako nje kwa dhamana.
Katika hatua nyingine, madiwani watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro akiwamo mwenyekiti wa halmashauri hiyo, wanashikiliwa na maofisa wa Kikosi cha Maalumu cha Kupambana na ujangili.

0 comments:

TULITENGWA MAONI YA SHERIA YA MABADILIKO KATIBA MPYA


Unaweza kujiuliza nani anasema kweli katika hili, hakuna shaka jibu litapatikana
Dar es Salaam. Wiki mbili baada ya Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi wa vyama vya CCM, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na UDP Ikulu mjini Dar es Salaam na kukubaliana mambo mawili makubwa kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, vyama visivyo wa uwakilishi bungeni vimeeleza kuwa havikushirikishwa katika kikao hicho.
Viongozi wa vyama hivyo vidogo waliibua hoja hiyo katika mkutano kati ya viongozi wa vyama vya siasa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi uliofanyika Dar es Salaam, kueleza kuwa Rais Kikwete alitoa kauli ya kutaka vyama vyote viwasilishe maoni, hakubagua chama chochote cha siasa.
Katika mkutano huo wa ndani, viongozi hao walimrushia  makombora mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wakidai kuwa yeye na wenyeviti wenzake wametoa maoni ya vyama vyao, siyo ya vyama vyote 20 vya siasa vilivyopo nchini na kwamba hawakushirikishwa.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, Peter Kuga Mziray (PPT Maendeleo) anasema kutokana na hali hiyo vyama  hivyo navyo vimeomba kuonana na Rais Kikwete ili kutoa maoni yake.
Jaji Mutungi kwa upande akalazimika  kutumia busara kupoza mvutano huo, huku akivionya vyama hivyo kujenga utaratibu wa kushirikishana katika kila jambo.
Katika mkutano wa Bunge uliopita wabunge wa Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala wa muswada huo bungeni  wakipinga matayarisho yake kutoshirikisha upande wa Zanzibar na pia walikuwa hawakubaliani na baadhi ya vipengele vya muswada huo.
Baada ya muswada huo kupitishwa, vyama hivyo viliungana na kutangaza kufanya maandamano makubwa, Oktoba 10 mwaka huu, ambayo hata hivyo hayakufanyika baada ya Rais Kikwete kuwaita Ikulu wenyeviti wa vyama hivyo na hatimaye kukubaliana.
Rais Kikwete na viongozi wa vyama hivyo walikubaliana kwamba vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili ifafutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya sheria hiyo.
Pia, walikubaliana kuwa  vyama vya siasa nchini viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano ili kusukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana ya nchi huku, huku Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)  kikipewa jukumu la kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.
Hali ilivyokuwa
Akitoa ufafanuzi wa jinsi vyama visivyo wa uwakilishi bungeni vilivyotoswa kutoa maoni yao, Mziray anasema: “Vyama vyetu ndani ya TCD vinawakilishwa na mwenyekiti wa UPDP, Fahm Dovutwa.

0 comments:

WAZAWA SASA KITENDAWILI CHAUMILIKI WA RASILIMALI

 
Rasilimali hapa nchini zipo kedekede, isipokuwa mgawanyo wake ndio umekuwa tatizo, huku wazawa wakiamini kuwa wageni wanapendelewa na kujengewa mazingira mazuri zaidi ya kuzifaidi.
Dar es Salaam. Tanzania ni nchi iliyojaliwa rasilimali nyingi na za kila aina.
Ina ardhi kubwa yenye rutuba, misitu , wanyamapori, madini mengi yakiwamo vito vya thamani na hata vyanzo vingi vya maji.
Hata hivyo, miaka 51 tangu ipate uhuru wake na ikiwa na idadi ya watu wapatao milioni 45, Tanzania bado ni miongoni mwa nchi maskini duniani.
Licha ya Serikali kubadilisha mfumo kutoka sera yake asili ya ujamaa na kujitegemea ambayo iliiwezesha kumiliki rasilimali zote hadi miaka ya 1980 na kuhamia kwenye mfumo wa soko huria, bado rasilimali zake hazijawanufaisha Watanzania.
Katika mfumo huria, kumekuwa na sera za uwekezaji ambazo zimewezesha watu wengi wenye mitaji  kutoka nje ya nchi kupewa rasilimali , kuzitumia kwa uzalishaji.
Tangu mwanzoni mwa mwaka 1990, kumekuwa na uwekezaji mkubwa zaidi katika sekta ya madini ambapo kampuni kubwa za madini duniani  zimemilikishwa migodi ya madini, hasa dhahabu.
Hata hivyo, kutokana na kasoro za hapa na pale, Tanzania bado haijafaidika na madini hayo huku maeneo mengi yanakochimbwa madini hayo yakikithiri kwa migogoro na umaskini mkubwa.
Kumekuwapo pia na uwekezaji katika sekta ya kilimo ambapo wawekezaji kutoka nje wamepewa maeneo makubwa ili kuendesha kilimo cha kisasa cha mashamba makubwa.
Kilimo hiki nacho hakijaifikisha nchi mahali pa kujivunia huku wakulima wengi wakiendelea na kile cha jembe la mkono.
Gesi na mafuta: Wapi tuendako
Hivi karibuni baada ya serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) imekuwa ikiainisha maeneo inakopatikana gesi asilia katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

0 comments:

JINSI KDF ILIVYOTIBUA UOKOAJI WESTGATE



Hadi sasa, Serikali haina habari yoyote ya ukweli kuhusu yaliyofanyika Westgate. Kamera za hivi punde zaonyesha baadhi ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) wakipora bidhaa kutoka katika maduka na benki ndani ya jengo la Westgate badala ya kuokoa watu.
Matarajio makubwa ya Wakenya yalikuwa kwamba jeshi lao litapambana na magaidi na kuwaokoa wananchi na mali zao, lakini matokeo yakawa kinyume.
Nairobi. Ni zaidi ya mwezi mmoja tangu Kenya ishambuliwe na magaidi wa Al-Shabaab.
Baada ya moshi kutokomea na waliouawa kuzikwa huku majeruhi wakiendelea kuuguza majeraha yao, maswali mengi bado hayajapata majibu.
Oktoba 18, runinga moja ya hapa nchini iliweka bayana kwenye habari zake jinsi mambo yalivyofanyika ndani ya jengo la Westgate tangu wavamizikuwasilia wakiwa wanaendesha gari ambalo walilinunua Septemba 6, mwaka kutoka kwa Mkenya mmoja ambaye hakujua kwamba alikuwa anawauzia watu wenye mpango mbaya.
Mpango ulivyosukwa
Kamera za usalama kwenye Benki ya Barclays iliyoko kwenye Barabara ya Mama Ngina, jijini Nairobi, zilinasa wavamizi wawili wakiingia kwenye benki hiyo na kutoa Sh365,000 (Sh6,840,000 za Tanzania) kutoka katika akaunti zao za kumlipa aliyekuwa amewauzia gari hilo.
Ndani la gari hilo siku ya tukio kulikuwa na wavamizi wanne ambao sasa majina yao yamejulikana baada ya uchunguzi wa kina wa ushirikiano wa Marekani, Israel na Uingereza kuwa ni Abu Baraa Al Sudani, Khatab Alakene, Umir Al Mogadish  na Omar Abdulraham Nabhan.
Wavamizi hao walikuwa wamepanga shambulizi hilo kwa umakini na wakafanikiwa kutekeleza kitendo chao cha kinyama bila kunaswa.
Si ajabu kwamba huenda walisaidiana na adui zetu kuvamia nchi ya mama yao. Tangu mwaka 2006 Kenya imekuwa ngome ya waasi ya al-Shabaab na mitandao yao ilikuwa imekita mizizi hasa katika eneo la Pwani, Kaskazini mwa nchi na Nairobi.
Jijini Nairobi, katika eneo la Eastleigh, asilimia 98 ya wakazi ni wenyeji wenye asili ya Somalia na ni kitovu cha Al-Shabaab nchini Kenya. Hapa ndipo ramani ya Westgate ilisomwa kwa makini na wavamizi walipokuwa wakijitayarisha kutekeleza maovu yao.
Inaaminika walipiga kambi kwenye nyumba mbili za wageni katika barabara za Eastleigh.  
Uvamizi huo ulifanyika peupe hivyo Polisi na Jeshi hawawezi kujitetea kwamba hawakuwa wanajua yote yanayopangwa na waasi wa al-Shabaab.

0 comments:

LAMPEDUSA ; KIVUTIO HATARI KWA WAHAMIAJI HARAMU...

  • Kisiwa cha Lampedusa hapo awali kilikuwa na wakazi 5,000, lakini katika miaka ya karibuni, pamekuwa pahala maarufu ambako Waafrika wanakimbilia. Mwaka huu pekee wameshawasili zaidi ya 30,000, lakini maelfu wengine wamezama baharini wakiwa katika safari hiyo ya hatari.  Wakimbizi hao wanaamini kwamba wakitia mguu Lampedusa ina maana wameshaukata, kama wanavosema vijana wa siku hizi au “wameshafika mtoni”.


Vijana wengi hutamani kwenda majuu bila kujua kwamba maisha ya huko si ya kutamani kama huna kazi ya kufanya.Matokeo yake wengi hupata matatizo na wengine kutoswa baharini.
Lampedusa ni kisiwa kidogo cha Italia katika Bahari ya Mediterranean, kikiwa na eneo la kilomita 21 za mraba na wakazi 5,000, hakiko mbali sana na mwambao wa Afrika Kaskazini.
Katika miaka ya karibuni, Lampedusa pamekuwa pahala maarufu ambako Waafrika wanakimbilia. Mwaka huu pekee wameshawasili zaidi ya watu 30,000, lakini maelfu wengine wamezama baharini wakiwa katika safari hiyo ya hatari.
Wakimbizi hao wanaamini kwamba wakitia mguu Lampedusa ina maana wameshaukata, kama wanavosema vijana wa siku hizi au “wameshafika mtoni” – Ulaya, wanayoifikiria kuwa ni peponi.
Mwanzoni mwa mwezi huu zaidi ya wakimbizi 300 walizama ndani ya boti iliyosheheni zaidi ya abiria 500 wakitoka Misrata, Libya.
Siku kumi baadaye wengine 26 walizama katika boti nyingine karibu na Kisiwa cha Malta wakitaka pia kufika Ulaya. Ni maafa ya kusikitisha na katika nchi za Umoja wa Ulaya kuna watu wengi wanaotaka iweko siasa mpya kuelekea wakimbizi, siasa ya kiutu.
Kiini cha tatizo
Lampedusa, kwa sura nyingine ni alama ya mizozo ambayo kiini chake ni serikali zinazotawala vibaya na kutowajali raia katika nchi kadhaa za Afrika
Wengi wa wakimbizi wa Kiafrika wanaovuka Bahari ya Mediterrenean na kwenda Italia wanatoka Somalia, Eritrea na Ethiopia. Utawala wa kidikteta wa Eritrea unawatisha na hauwapi nafasi raia kupumua.
Huko Somalia zaidi ya miaka 20 hakujakuweko na serikali ya maana. Wakimbizi wa kutoka nchi nyingine za Afrika wanatafuta hifadhi Ulaya wakichoshwa na hali duni ya kuwa na mustakbali bora wa maisha. Wanahisi ni bora wajichovye na waelekee hata kusikojulikana, licha ya hatari nyingi zilioko mbele yao.
Utaona familia nyingi za Kiafrika huchanga fedha angalau mmoja wa vijana wao ajitose na asafiri hadi Ulaya kama mkimbizi na huko akatafute maisha. Matarajio ni kwamba pindi kijana huyo atafanikiwa basi huenda atapeleka nyumbani fedha na kuwafaidisha jamaa zake.
Hata hivyo, kwa vijana wengi mambo hayaendi kama walivyoyatazamia. Fedha walizochangiwa humalizikia katika mikono ya walanguzi makatili ambao ni mawakala wa safari hizo za magendo.

0 comments:

TEGETE NI MFUNGAJI MZURI BADO ILA AMEKOSA UMAKINI TU




Na Baraka Mbolembole
" Ni kweli sisi wachezaji tunajua kuwa mashabiki wanazipenda timu zao, hasa kwa wale wa timu yetu ya Yanga tunajua wanaipenda sana timu yao, lakini nawashauri wabadilike sasa, wasiwazomee wachezaji wakati wanapokuwa wanafanya vibaya. Wawe na subira kama kweli wanaipenda timu yao. Kelee zao huwatoa mchezoni wachezaji na kujikuta wakifanya vibaya zaidi, na hili hupelekea hata kwa wale wachezaji wanaokuja kuingia katika uoga, nawasihi wawe na uvumilivu"
Ni maneno ya mshambuliaji aliye katika wakati mgumu hivi sasa katika klabu ya Yanga, Jerry Tegete, wakati nilipofanya nae mazungumzo hivi karibuni kuhusiana na mwenendo wake usiovutia hadi sasa katika klabu hiyo.

Jerry ambaye alianza vizuri msimu huu pale alipofunga maba mbili siku ya ufunguzi wa msimu dhidi ya Ashanti United, na akafunga tena katika mchezo uliofuata hila amekuwa akipoteza nafasi za wazi mara kwa mara na kupelekea ,kuwakera wengi.
Wakati ushindani wa kuwania nafasi ukiwa ni mkubwa katika safu ya mashambulizi ya Yanga, ambayo imekusanya washambuliaji sita wa kati na wengine wawili wakiwa kama viungo washambuliaji, Jerry amejikuta akipoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza, na katika siku za karibuni amekuwa akikosa hata nafasi ya kuingia kama mchezaji wa akiba.

Didier Kavumbagu, ameoneka kuwa chaguo la kwanza mbele ya kocha, Ernie Brandts, na Mrundi huyo ameweza kuwa kiongozi wa safu yote ya mashambulizi, nguvu, akili na uwezo wa kumiliki mpira, unaambatana na umakini mkubwa wa kutumia nafasi anazotengenezewa, ' Kavu' amekuwa chaguo bora mbele ya Tegete katika vitu vingi, mwanzoni mwa msimu walipangwa walikuwa wakipangwa pamoja na wakaonekana kuwa wafungaji wazuri, walifunga kwa vichwa, na uwezo binafsi na matokeo yake wakawa chaguo la kwanza.
" Ushindani ni mkubwa sana, na nafasi imekuwa ni ngumu, kila mchezaji hutumia nafasi anayopata vizuri" anaongeza, Tegete. 'Kavu', Tegete, Said Bahanunzi, Hussein Javu, Kondo awali walikuwa washindani wa kwanza katika nafasi hii, ila kurejea kwa Hamis Kizza aliyekuwa kwenye majaribio nchi ya ng'ambo, na kumalizika kwa adhabu ya Mrisho Ngassa kumefanya hali ya mambo kuwa magumu zaidi.
Lakini inakuwaje kwa mchezaji kama Jerry kuzomewa mara kwa mara na mashabiki wa timu yake? Wakati fulani hali hii iliwahi kumtokea kiungo wa zamani wa timu hiyo, Nurdin Bakari, hasa pale alipokuwa akifanya vibaya uwanjani, kila mtu alikuwa anafahamu uwezo wake, lakini pasi mbili au tatu tu ' mbovu' uwanjani zilikuwa ni tatizo. Kitu kizuri huleta furaha ya siku zote katika maisha, ni shida sana kukishusha chini kitu kizuri, mafanikio hayahitaji kubweteka na kupelekea mtu kujisahau kule alipotoka na alipokuwa amepanga kufikia, umakini, nidhamu ya mchezo, huwa ni sehemu ya mipango mizuri ya wachezaji wote waliofanikiwa. Wapo ambao walipitia njia ya kupingwa na kuzomewa na mashabiki wa timu zao ila bado wakafanya kazi nzuri uwanjani na kujikuta wakifanikiwa.

Dr. Martin Luther King Jr aliwahi kusema; " Ukimya wa rafiki yako unaumiza sana kuliko kelele za adui yako" pengine, manaharakati huyu wa haki za binadamu, na aliyekuwa mtetezi wa watu weusi katika Marekani, alikuwa na maana nyingi lakini ni vyema wakati mwinmgine wachezaji kama Tegete wakachukulia kelele za zomea zomea za mashabiki wao ni sehemu za kuwakumbusha kuwa hawafanyi vizuri. Na mashabiki hawatakiwi kufanya hivyo mara kwa mara klwa kuwa mara moja au mbili inatosha kufikisha ujumbe kwa muhusika.

Katika miaka mitatu ya karibuni, Tegete amekuwa akikumbwa na majeraha ya mara kwa mara, na hajawahi kucheza michezo sita mfululizo ndani ya misimu mitatu sasa klabuni kwake.
" Namshukuru Mungu kwa kila jambo, nashukuru hivi sasa nimepona goti, hilo ndilo lilikuwa ni la muhimu sana kwangu. Unajua hata sisi wachezaji hatupendi kufanya vibaya, wakati wa mchezo na Simba niliumia na kusikitika sana kwa sababu hadi nusu ya kwanza tunaongoza 3-0, kipindi cha pili wakarudisha goli zote.

Niliumia sana goli kurudi na nilikuwa nina imani tungeweza kuongeza bao lingine muda wowote. Simba walijitahidi sana" . Hili ni kweli kuwa hakuna mchezaji anayependa kufanya vibaya na wakati mweingine matokeo yao mabaya uwanjani hutokana na uwezo mzuri wa timu nyingine. Ila mimi binafsi nahitaji mabao kutoa kwa Tegete, nimechoka kumuona akipoteza nafasi rahisi mara kwa mara mchezoni, ila ujumbe wangu kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba, ' Muacheni, Jerry acheze mpira sasa, baaada ya kucheza walau michezo mitao hadi saba mfululizxo mnaweza kumuhukumu' . Tegete ni mfungaji mahiri bado, amekosa umakini tu kama aliona nao Kizza au Kavumbagu.

0 comments:

YANGA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU - YAIPIGA MGAMBO 3-0



Kikosi cha Young Africans kilichoanza dhidi ya Mgambo Shooting
Young Africans mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu Tanzania bara leo wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa timu ya Mgambo Shooting kutoka mkoani Tanga kwa mabao 3-0, mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Ikiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Rhino Rangers kwa mabao 3-0, kikosi cha Young Africans kiliingia uwanjani kwa lengo la kuendeleza wimbi la ushindi na ndivyo hali ilivyokuwa

Hamis Kiiza, Saimon Msuva na Mrisho Ngasa walikosa mabao ya wazi dakika 15 za kipindi cha kwanza kufuatia kutokua makini katika umaliziaji na kujikuta mipira yao ikitoka pembeni mwa lango la Mgambo Shooting na mingine ikiokolewa na golikipa wa Mgambo Shooting Tonny Kavishe.

Mbuyu Twite aliipatia Young Africans bao la kwanza Young Africans dakika ya 31 ya mchezo kwa shuti kali la mita 25 kwa mpira wa adhabu alioupiga na kujaa moja kwa moja wavuni na kuamsha shangwe kwa washabiki wa Yanga.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 1 - 0 Mgambo Shooting.

Kipindi cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo aliingia nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' kuchukua nafasi ya Rajab Zahir mabadiliko ambayo yaliongeza uwezo wa kumiliki mchezo na kulinda vyema lango lao.

Dakika ya 50 ya mchezo, Hamis Kiiza 'Diego' aliipatia Young Africans bao la pili kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinda mlango wa Mgambo Shooting Tony Kavishe kumuangusha Didier Kavumbagu ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambayo Kiiza hakufanya makosa.

Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans bao tatu la mchezo dakika ya 67 ya mchezo baada ya mpira uliorushwa na mlinzi Mbuyu Twite kumkuta Kavumbagu ambaye aliwazidi maarifa walinzi wa Mgambo Shooting na kuukwamisha mpira wavuni.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 0 Mgambo Shooting.

Msimu uliopita katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kati ya timu hizi Young Africans pia iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, mabao yaliyofungwa na Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na Nadir Haroub 'Cannavaro'

Young Africans: 1.Dida, 2.Twite 3.Oscar, 4.Rajab/Cannavaro 5.Yondani, 6.Chuji, 7.Msuva/Lusajo 8.Domayo, 9.Kavumbagu, 10.Ngassa, 11.Kiiza

0 comments:

URAISI WA TFF - RAISI WA CAF ISSA HAYATOU AMPONGEZA JAMAL MALINZI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.

Amesema CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.

Rais Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.

0 comments:

SIMBA KURUDISHA MAKALI YAKE LEO DHIDI YA KAGERA SUGAR???


SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANALEO
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 leo (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

PAMBANO LA YANGA, MGAMBO SHOOTING LAINGIZA MIL 37/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa jana (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 37,915,000.

Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati kila klabu ilipata sh. 8,550,741.95.

Wamiliki wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh. 2,608,700.93, Bodi ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,304,350.47, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,014,494.81.

0 comments:

SIR ALEX FERGUSON AVUNJA REKODI NYINGINE - MAUZO YA KITABU CHAKE YAFUNIKA

Hot cakes: Fergie's book has been a quick seller
Hot cakes: Fergie's book has been a quick seller

REUTERS
Kitabu cha Sir Alex Ferguson kimeweka rekodi ya kuwa kitabu kilichooza kwa haraka zaidi ndani ya Uingereza kikiuza nakala 115,547 katika siku chache za mauzo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Bookseller, kitabu hicho cha mocha wa zamani wa Manchester United kimevunja rekodi ya  Delia Smith,  ambaye kitabu chake cha mwaka 1999 cha mapishi kiliuza kopi 112,000 katika wiki take ya kwanza.

Pia kitabu cha Fergie kimevunja rekodi ya mauzo ya kitabu cha rafiki yake waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair, ambacho kiliuza kopi 92,000 katika wiki ya kwanza.

VITABU VILIVYOUZA ZAIDI UK:
Sir Alex Ferguson - My Autobiography - 115,547
Delia Smith - How to Cook - book two - 112,000
Tony Blair - A Journey - 92,000
David Beckham - My Side - 86,000
Paul Burrell - A Royal Duty - 77,000

0 comments:

MKUTANO WAKILELE WA UMOJA WA ULAYA

Viongozi wa serikali na nchi 28 za Umoja wa Ulaya wanakutana kwa siku mbili mjini Brussels ikiwa ni wiki kadhaa baada ya janga la kuangamia wakimbizi katika kisiwa cha Lampedusa.
Kansela Merkel , rais wa baraza la EU Herman Van Rompuy na Mkuu wa sera za nje za EU Catherine Ashton Kansela Merkel , rais wa baraza la EU Herman Van Rompuy na Mkuu wa sera za nje za EU Catherine Ashton
Katika mwaliko wa mkutano wa kilele uliotolewa na rais wa baraza la Umoja wa Ulaya, Herman Van Rompuy, suala la wakimbizi katika ulaya ya Kusini limetajwa kwa mukhtasari tu. Aidha katika maazimio ya mkutano huo wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels ambayo tayari yameshatolewa kama rasimu, kisa cha Lampedusa katika bahari ya Mediterenia hakijachukuwa dhima kubwa. Viongozi wa serikali na nchi 28 za Umoja wa Ulaya wanakutana kwa siku mbili mjini Brussels. Mkutano huu unafanyika baada ya janga la kuangamia wakimbizi katika kisiwa cha Lampedusa kuzusha sauti za ukosoaji kuelekea sera ya Umoja wa Ulaya katika suala hilo la wakimbizi.
Suala la wakimbizi
Kwa waziri mkuu wa Italia, Enrico Letta hatua za Umoja wa Ulaya kuelekea suala hilo la wakimbizi hazitoshi. Baada ya mamia ya wakimbizi kuzama kufuatia ajali ya boti waliyokuwa wakisafiria katika kisiwa cha Lampedusa mwezi huu, waziri mkuu huyo wa Italia anatazamiwa kuwatia shime viongozi wenzake kutafakari suala la kugawana wakimbizi barani Ulaya.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika mojawapo ya mikutano yao ya kilele Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika mojawapo ya mikutano yao ya kilele
"Kuna baadhi ya nchi ambazo zinatuunga mkono. Baadhi ya nyingine zinafanya mambo kinyume na tunavyofanya sisi. Ni kwa nini tunataka suala hili lishughulikiwe katika ngazi ya Ulaya ni kwa sababu ndiko tunakofikia msimamo wa pamoja. Kwa mfano katika mwaka wa 2014 wakati Ugiriki na Italia zitakapochukuwa uwenyekiti wa Umoja wa Ulaya pamoja na kamisheni ya Umoja huo na baraza zitabidi kufanya kazi kwa pamoja kushughulikia suala hili''
Kauli ya Letta imetolewa wiki moja baada ya mkasa wa Lampedusa pale walipotembelea pamoja na rais wa Halmashauri ya Umoja huo, Jose Barroso, kisiwa hicho cha Italia kilichoko nje ya pwania ya Afrika Kaskazini.
Ujerumani pamoja na baadhi ya nchi nyingine za Ulaya Kaskazini zinatarajiwa kudokeza katika mkutano huo juu ya suala la taratibu za uhamiaji katika Ulaya ambazo zilidurusiwa katika kipindi cha msimu wa joto. Nchi hizo zinategemewa kuzungumzia kile kinachojulikana kama sheria za Dublin ambazo kimsingi zinawalazimisha wanaoomba ukimbizi kuomba kinga katika nchi ya kwanza waliyofikia.
Misimamo
Duru kutoka serikali ya Ujerumani zimedokeza kabla ya mkutano huu wa kilele kwamba tayari limeshaundwa jopo la maafisa wa Umoja wa Ulaya pamoja na mawaziri ambao watakutana hii leo kwa mara ya kwanza likiwa na jukumu la kutowa ushauri juu ya njia zinazostahili kufuatwa katika suala la uokozi wa baharini na kuhusu ushirikiano wa karibu na nchi ambako wanatokea wakimbizi wanaoingia Ulaya.
Kisiwa cha Lampedusa - August 20, 2009 kiasi wakimbizi haramu 75 kutoka Afrika walifariki Kisiwa cha Lampedusa - August 20, 2009 kiasi wakimbizi haramu 75 kutoka Afrika walifariki
''Nataraji kwamba Halmashauri ya Umoja wa Ulaya itafunguwa njia ya kupatikana msimamo wa pamoja wa uwajibikaji pamoja na sera ya kudhibiti uhamiaji katika kiwango cha Ulaya. Hakuwezi kuweko miujiza au mafanikio ya haraka haraka kwa sababu tatizo ni kubwa na linahitaji hatuwa madhubuti kuokowa maisha ya watu''
Kwa upande wa Ujerumani Martin Schulz ambaye ni rais wa Bunge la Ulaya kutoka chama cha SPD amedai mara kadhaa katika mahijiano kwamba Ujerumani inabidi kubeba jukumu kubwa la kuwapokea wakimbizi zaidi pamoja na wahamiaji ambao wanazidi kuingia Ulaya kwa kupitia bahari ya mediterenia.Hata hivyo waziri wa mambo ya nje anayemaliza muda wake Guido Westerwelle kutoka FDP amekiri katika mkutano uliopita wa mawaziri huko Luxembourg siku ya Jumatatu Ulaya haipaswi kupuuza tatizo hili.
''Ulaya haipaswi kuangalia kando na kupuuza .Hii ni hali ngumu na sio tu kwa nchi husika lakini ni tatizo hata kwa watu wanaohusika katika tatizo hili.Nataraji kwamba agenda hii itajadiliwa katika mkutano huu wa Kilele.Hili ni suala lisiloweza kuepukika.''
Uchumi
Aidha masuala ya kiuchumi pia yanatazamiwa kuzungumziwa kwa kina katika mkutano huo huku suala la mikataba ya mafungamano ya pamoja ya tume ya Umoja wa Ulaya likitarajiwa kuchukuwa nafasi ambapo Ujerumani inapania kupigia debe mageuzi kadhaa wakati baadhi ya nchi zikiwa na msimamo wa kuikosowa hatua hiyo.
Mwandishi/Riegert, Bernd (DW Brüssel)/Saumu
Mhariri:Josephat Charo

0 comments:

Lack of sleep can cause weight gain of 2 pounds (0.9 kg) in under a week.

Some Deaf People Make Sign Language in TheirSleep

0 comments:

SERIKALI KUWAPA WAKULIMA MIEZI MITATU NI VICHEKESHO

 
Hivi karibuni, wakulima wa mahindi mkoani Rukwa walipasua jipu kwa kuilalamikia Serikali kuhusu kitendo chake cha kuwakopa mahindi yao tangu Julai mwaka huu na hadi sasa haijawalipa.
Wakulima hao walitoa kauli zao kupitia vyombo vya habari, ambapo walilalamika kwa sauti za kukata tamaa kwa Serikali yao na kusisitiza kwamba wamechoka kuvumilia.
Ilielezwa kwamba Serikali kupitia Wakala wa Hifadhi ya Chakula cha Taifa iliwakopa wakulima lukuki wa mkoa huo tangu Juni, huku ikiwaahidi kuwalipa mapema Agosti.
Wakulima wa mkoa huo wanaidai Serikali zaidi ya Sh6 bilioni na mpaka sasa haijataja ni siku gani wakulima hao watalipwa.
Hali kadhalika wakulima wa zao hilo mkoani Ruvuma nao wametoa ya moyoni wakiilalamikia Serikali kwamba iliwakopa mahindi tangu Juni hadi sasa haijawalipa.
Meneja wa Wakala wa Hifadhi ya Chakula cha Taifa mkoani Ruvuma, Morgan Mwaipyana alikiri kwamba wakulima kudai zaidi ya Sh5 bilioni za mahindi waliyoikopesha Serikali.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu alisema Serikali ililazimika kuwakopa wakulima, baada ya mahindi yao kuwa mengi kuliko makisio ya manunuzi.
Alisema kwa miezi miwili waliweza kukusanya zaidi ya tani 55,000 za mahindi ya wakulima wakati malengo yalikuwa chini ya tani hizo.
Sawa, pamoja na mambo mengi ambayo wakulima wanailalamikia Serikali, lakini suala la Serikali kuwakopa wakulima mazao yao kwa muda mrefu halieleweki kabisa.
Je, ni nani ama mfanyakazi gani wa Serikali asiyetambua jasho la mkulima linavyotoka akiwa shambani mpaka anadiriki kuchelewesha fedha za mkulima?
Ni nani asiyejua jinsi wakulima wanavyodamka asubuhi mapema na kujiingiza kwenye udongo kwa siku nzima wakibugia vumbi ama tope, wakilowa mvua ama kupigwa na jua ili kupata mavuno?
Je, wafanyakazi wa Serikali wanaochelewesha fedha za wakulima hao wana nia gani kwa chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015?

0 comments:

VIONGOZI CHADEMA WAZIPIGA KAVUKAVU KWENYE MKUTANO WAMBOEWE ARUSHA

0 comments:

POLISI 56 WAFUKUZWA KAZI KWA MAKOSA YA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA


JESHI la Polisi nchini limewafukuza kazi askari wake 56 katika kipindi cha mwaka mmoja, kutokana na makosa ya kuomba na kupokea rushwa pamoja na utovu wa nidhamu.Kamishna msaidizi wa jeshi hilo, Patrick Byatao, alisema hayo jana alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali hususan masuala ya nidhamu kwa askari wake katika warsha ya siku maalumu ya polisi iliyofanyika mjini Bukoba.
Alisema kuwa askari waliofukuzwa ni kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ambao wamekutwa na tuhuma za utovu wa nidhamu ikiwemo kuomba rushwa kwa wananchi. Kwa kipindi cha mwaka 2012, waliwafukuza askari 35 na mwaka huu 21.
Kwa mujibu wa Byatao, wapo baadhi ya askari ambao wamekuwa wakitoa visingizio vya kuomba rushwa kwa sababu mishahara yao ni midogo na haitoshelezi mahitaji yao.
 
Alisema ni heri askari wa aina hiyo wakaacha jeshi, vinginevyo wataendelea kuchukuliwa hatua kama hawatafuata masharti ya kazi yao.

Akitoa mada juu ya kuimarisha maadili ndani ya jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka makao makuu, Andrew Makungu, alisema wameanzisha mkakakati wa kudhibiti vitendo vya ukiukwaji maadili kwa askari wake ikiwemo rushwa.
 
Alitaja maeneo lengwa kuwa ni chumba cha kupokea taarifa za mashitaka, usalama barabarani na upelelezi wa makosa ya jinai. Bado juhudi zinaendelea ili kuboresha maeneo mengine.
 
Makungu alisema ubia wa kiutendaji wa jeshi hilo umekuwa ukiimarika kila siku baada ya sehemu kubwa ya jamii kutambua nafasi yao katika jukumu hilo. 
 
Alisema mambo hayo yanaonekana kutokana na wananchi kufanya ulinzi wa maeneo yao, kuchangia rasilimali kwa jeshi, kutoa taarifa sahihi za uhalifu, kujenga vituo vya polisi na kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi. Hadi sasa viko vikundi 5,344 nchi nzima huku Mkoa wa Kagera ukiwa na 431.
 
Naye mgeni rasmi katika warsha hiyo, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, alisema kuwa Jeshi la Polisi limekuja na mkakati wa polisi jamii/ulinzi shirikishi unaoelekeza kuwapo kwa mashauriano, majadiliano ya kiutendaji yanayosisitiza uwepo wa maadili katika kazi, ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa ndani ya jamii.

0 comments:

CHADEMA WASHIKANA MASHATI HUKO JIJINI ARUSHA.....MBOWE AIVURUGA BAADA YA KUDAIWA KUIBA MILIONI 80 ZA CHAMA..!!


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kanda ya Kaskazini, kimemsimamisha Uongozi Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa  wa Arusha Samson Mwigamba kwa madai ya kukihujumu chama hicho. 
 
Taarifa ambazo tumezipata kutoka ndani ya kikao cha Baraza la uongozi kanda ya Kaskazini, kilichofanyika katika Hotel ya Corridor Spring leo usiku, zimedai uamuzi wa kusimamishwa Mwigamba umefikiwa na Kikao hicho baada ya kuwasilishwa kwa vielelezo kadhaa vya Mwigamba na yeye kukiri  kuwa ni vyake huku vingine vikimuonyesha kuwa ndiye mmiliki wa Akaunti ya Jina la ‘Maskini Mkulima’ ambalo limekuwa likitumika kukichafua chama kwenye mitandao ya kijamii.
Hakuna kiongozi ambaye amekuwa tayari kuzungumzia suala hili kiofisi, lakini taarifa za uhakika ambazo tumezipata kutokana  na maamuzi ya kikao hicho  zimebainisha kuwapo kwa maamuzi hayo pasipo shaka.
  “Kikao hicho kimemsimamisha Uongozi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili, hivyo kuanzia sasa mwigamba siyo kiongozi, nadhani tamko litatolewa baadaye,” alieleza mmoja wa wajumbe wa kikao  hicho kilichofanyika  Arusha na kuongeza kuwa katika Kompyuta yake baadhi ya maandiko ambayo yamekuwa yakikikashfu chama yamekutwa ikiwa ni pamoja IP address ya Jina na Maskini Mkulima ambalo limekuwa likituma post ndani ya Jamiiforums kukuta zinafanana.
Jina la ‘Maskini Mkulima’ lilijiunga na mtandao wa jamiiforums mnamo Desemba 27, 2011 na mpaka jana inaonyesha alikuwa ametuma zaidi ya Post 27 ikiwamo hii iliyokuwa na kicha cha habari: Wito kwa wana CHADEMA wote.
 

Makala hiyo ambayo ndiyo imefanikisha kumbaini ilitumwa Jamiiforums Oktoba 19 Mwaka huu chini ya kichwa cha habari cha ‘Wito kwa wana CHADEMA wote!’, inaeleza haya;
 

Kufuatia malumbano yanayoendelea kwenye vyombo vya habari na madhaifu mengi ambayo tumeshayashuhudia kwenye chama kwa sasa, natoa wito kwa wana CHADEMA wote nchini kwamba wakati umefika tubadilishe uongozi wa juu wachama.
 

Kihistoria, CHADEMA kati ya mwaka 2005 na 2010, agenda zetu kwa wananchi zilikuwa mbili. Kupiga vita ufisadi, iliyosukumwa sana na Dr. Slaa na ile ya utetezi wa raslimali zetu iliyobebwa na Zitto. Lakini sasa hivi chama kinaenda kwa matukio.
 

Naandika nikiwa mwana CHADEMA safi na nataka kila mwanachama atakayesoma atulie na kutafakari. Hili siyo jambo la ushabiki. Nimawasiliano baina yetu wana chadema na tunahitaji tutulie na kutafakari.
 

Nimekuwa mwanachama wa siku nyingi na nimebahatika pia kuwa kiongozi ndani ya chama kwa nyakati tofauti kwahiyo naelewa ninachokiandika.

 Nadriki kusema kwamba kwa sasa chama kinakwenda kwa matukio na ni bahati tu kwamba CCM inaendelea kutupatia matukio lakini CCM na serikali yake wakitunyima matukio, CHADEMA chini ya Mkt Mbowe, Katibu mkuu Slaa na Naibu Zitto utakuwa ndo mwisho wake.
 

CHADEMA iliyopiga kelele sana dhidi ya ufisadi, CHADEMA iliyopiga kelele mpaka sheria ya vyama vya siasa ikabadilishwa na vyama kutakiwa kukaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), eti leo inaungana na CCM kumshambulia mwenyekiti wakamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC) kwa kutamka kwamba vyama havijawasilisha ripoti zake za fedha zilizokaguliwa. Kwa nini? Muungano huu wa CHADEMA na CCM maana yake nini? 
 

Kama chama kinajiamini ni kisafi kwenye hesabu zake hofu ni ya nini? Si wasubiri kikao na kamati ya bunge katibu mkuu aende na hizo ripoti na nyaraka zinazoonyesha kweli wamewasilisha hesabu hizo?
 

Napenda kabla sijaendelea mbele kuwapongeza wenyeviti wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wakutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. 

Hawakuwa madikteta na nawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwanachama.
 

Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika katiba yetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea nakuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada ya hapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili.

 Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika katiba bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.
 

Napenda pia kumpongeza mwenyekiti aliyepo madarakani, Mbowe. Kuna mengi kakifanyia chama. Kakitoa kutoka kwenye chama cha tatu ama nne kwa upinzani hadi kuwa cha kwanza na kustahili kuitwa chama kikuu cha upinzani. 

Kakichukua kikiwa na wabunge 5 bungeni na leo katika kipindi chake cha miaka 10 kina wabunge 49.

 Ni achievement kubwa! Si hivyo tu, ni wakati wake CHADEMA imebeba agenda nzito za kitaifa kama vile vita dhidi ya ufisadi, utetezi wa raslimali, katiba mpya,nk.
 

Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Ni muhimu kwa Mbowe kuelewa kwamba uwezo wake umefikia hapo asitake kulazimisha kusonga mbele akidhani bila yeye hakuna CHADEMA. 

Akiache chama kikiwa salama, abaki kama mwenyekiti mstaafu na awaachie wengine awamu inayofuata ya kuingia madarakani. Kama hataki kuwa mwelewa na kuachia ngazi, wanachama tumsaidie kwa kumpiga chini uchaguzi ujao.
 

Leo nitaainisha mambo machache tu yanayohusiana na fedha za chama na uaminifu ili wanachadema muelewe kwa nini viongozi wakuu wa chama wamehamaki sana kusikia wanatakiwa kuwasilisha ripoti za fedha wakajikuta wanapambana na mwenyekiti wa kamati ya bunge badala ya kamati na hata kufikia kusahau kwamba huyo mwenyekiti wa kamati ya bunge ni mwenzao, ni naibu katibu mkuu wa chama. Mengine nitaendelea kuyadondoa siku nyingine nitakapopata fursa:
 

1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano. 

Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. 

Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.
 

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. 

Kama kingekuwepo leo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi.

 Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe,  bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.
 

2. Matumizi ya fedha za chama:

Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani Mwenyekiti Taifa, katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha.

 Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. 
 

Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha Baraza kuu cha mwezi January kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa, wilaya namajimbo na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa 10 maamuzi hayo hayajatekelezwa ipasavyo.
 

Nyinyi viongozi wa kanda,mikoa, wilaya na majimbo ni mashahidi wa hili . Lakini kuna michango ya watu binafsi kama Mzee Sabodo, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. 

Hapo sijataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es Salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.
 

3. Taarifa za fedha

Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za chama. 

Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu niliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. 

Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama.
 

 4. Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama
 

Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. 
 
Mawazo mazuri kama la kuanzisha kampuni la uwekezaji la chama litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana. 

Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa Kenya juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.
 

5. Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi
 

Chama chetu kinayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya sekretariat. Lakini kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu,wamekubali kuzimwa.

 Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, kadi za uanachama, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa katibu mkuu, hawana. 

Manunuzi haya yote yanafanywa na wakuu bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Hivi tunavyoongea, ni mwenyekiti taifa mwenyewe ndiye aliyenunua magari na pikipiki zote za M4C.
 

Hivi tunavyoongea kuna shilingi milioni 80 ambazo mwenyekiti taifa alizichukua na kuagiza kadi za uanachama tangu mwaka jana mpaka leo hizo kadi hazijawahi kuonekana. 

Na mwenyekiti anafanya mambo hayo yote akitambua kwamba yeye ni mwenyekiti na hayo ni masuala ya kiutendaji ambayo yako chini ya katibu mkuu kama mtendaji mkuu wa chama na kamati yake ya tenda. Huu si ufisadi ni nini?
 

6. Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya uenezi vya chama

Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya chama na chama kinanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya chama kama bendera vinauzwa na mtu binafsi. Jambo hili linajulikana kwa Mwenyekiti Taifa na Katibu Mkuu wake tu. 

Napenda kwanza kuipongeza kamati ya bunge kwa kuvikomalia vyama vinavyopokea ruzuku bila kujali ni chama tawala ama pinzani.
 

Pili namshauri CAG unaweza kutumia kampuni binafsi kwenye wizara, idara, taasisi, wakala, na asasi zote za kiserikali na serikali za mitaa kwenye ukaguzi lakini kamwe usiruhusu vyama vya siasa vikaguliwe na kampuni hizo. 

Hapo nenda mwenyewe ndo utajionea mwenyewe. Kampuni binafsi kwenye vyama huko zinafundishwa ziandikeje maoni yao. Nenda mwenyewe ujionee.
 

Pia kuna mkakati unaendeshwa na CHADEMA Makao Makuu kwa sasa wa kuwapigia simu viongozi wa mikoa hasa hapa Dar es Salaam na mikoa mikubwa kama Mwanza, Arusha, Mbeya, nk, wakiwataka viongozi wa mikoani mtoe matamko kumpinga Zitto. Kataeni ushenzi huu. Hili si jambo la Zitto ni la kamati ya bunge na kimsingi ni la uadilifu ndani ya serikali na vyama. 
 

Hata kama jambo lenyewe lingekuwa limeagizwa na Mwigulu Nchemba msingetoa matamko ya kupinga zaidi ya kuwaacha viongozi wetu wakuu watoe ripoti kuthibitisha uadilifu wao japo kidogo maana ni ukweli pia kwamba kwenye ripoti wanaweza kuzuga zikawa safi lakini ufisadi umefanyika. 
 
Kama ni matamko toeni matamko ya kuutaka uongozi wetu utoe hizo ripoti, na hapo ndipo mtakapo jua kwanini hampati ruzuku. Kuna matumizi mengi sana ya hovyo na ufisadi mkubwa unafanyika hapo Makao Makuu.
 

Nitaendelea kuwadondolea ili muone kwa nini napendekeza tuung'oe uongozi huu chini ya Mbowe.

Ahsanteni kwakunisoma!
Masikini Mkulima

0 comments: