Jenerali Mwamunyange alisema wanajeshi hao
waliuawa wakati wakisafiri kutoka eneo la Khor Abeche kwenda Nyala wakisindikiza
msafara wa waangalizi wa amani wa Umoja wa Mataifa (UN).
“Ilikuwa ni Julai 13, saa tatu asubuhi na
walipokuwa wamesafiri umbali wa kilometa 25, walifika kwenye eneo lililokuwa na
mteremko mkali na lenye utelezi kufuatia mvua kubwa iliyokuwa imenyesha. Ilibidi
wapunguze mwendo wa magari yao ili yaende taratibu, kumbe ndiyo walikuwa
wanaingia kwenye ‘ambush’ na kujikuta wakishambuliwa,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo, ilibidi wapigane
kwa weledi mkubwa kwa karibu saa mbili ili kujinasua toka kwenye ambush hiyo,
hadi pale walipopata msaada kutoka kwa askari wenzao waliokuja
kuwasaidia.
Alisema kutokana na juhudi za kupigana kwa
weledi kwa lengo la kujinasua, ilibidi waasi wakimbie, lakini tayari wakiwa
wameshaua mashujaa hao saba na kujeruhi wanajeshi wengine 14, kati yao akiwamo
ofisa mmoja wa polisi.
HALI
ILIVYOKUWA
Shughuli ya kuaga miili ya mashujaa hao saba,
Sajini Shaibu Othman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Ally, Koplo Mohamed
Chikilizo, Private Fortunatus Msofe, Private Rodney Ndunguru na Private Peter
Werema, ilianza saa tatu asubuhi kwa kuwasili wageni mbalimbali, wakiwamo
mawaziri, mabalozi wanaowakilisha nchi zao na maofisa wa UN, maofisa waandamizi
wa serikali, wakuu wa majeshi wastaafu na wanadhimu wastaafu.
Pia walihudhuria majenerali wastaafu,
majenerali walio kwenye utumishi, wafanyabiashara, akiwamo Dk. Reginald Mengi,
familia za wafiwa na wananchi wa kada zote.
VIONGOZI WA KITAIFA
WAWASILI
Majira ya saa nne asubuhi, Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi aliwasili, akifuatiwa na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal aliyewasili saa
4:52.
KIKWETE
AWASILI
Rais Jakaya Kikwete aliwasili saa 5:08 asubuhi
na shughuli ya kuileta miili ya mashujaa kwenye viwanja hivyo vya Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga, jijini Dar es salaam
ilifuata.
MIILI
YAWASILI
Lilianza gari lenye namba 5914 JW 12 lililokuwa
limebeba jeneza la Sajini Othman, ambalo lilingia majira ya saa tano na robo
asubuhi.
Jeneza hilo lilishushwa na askari wanane wenye
vyeo vya sajini wakisindikizwa na askari wawili na kisha kupeleka jeneza hilo,
juu ya meza moja maalumu iliyokuwa imeandaliwa.
Hatimaye lilifuata gari namba 5980 JW12
lililokuwa na jeneza la mwili wa Koplo Chaula, lililoingia saa 5:19, kisha gari
namba 5907 JW12 lililokuwa na mwili wa Koplo Chikilizo, lililoingia saa 5:23 na
gari namba 5913 JW12 lililioingia saa 5: 27, likiwa na mwili wa koplo
Ally.
Baadaye lilifuata gari namba 5912 JW12
lililoingia saa 5: 32, likiwa na mwili wa Private Msofe, kisha gari namba 5976
JW12 lililoingia saa 5:36, likiwa na mwili wa Private Ndunguru na mwisho gari
namba 5906 JW 12, likiwa na mwili wa Private Werema.
AMIRI JESHI
AONGOZA
Rais Kikwete aliongoza waomboleza wote kuaga
miili hiyo mnamo saa 5:47 pale alipopita mbele ya majeneza yaliyokuwa
yamefunikwa kwa bendera ya taifa na kisha akamalizia kwa kuwapa mkono wa pole
familia za wafiwa.
Baadaye Makamu wa Rais, Dk. Bilal alifuata
akiwaongoza viongozi mbalimbali waliokuwa kwenye turubai kuu, wakiwamo mawaziri,
mabalozi, maofisa wa UN, maofisa waandamizi wa serikali, majenerali wastaafu na
maofisa wakuu walioko jeshini.
RISALA ZA
RAMBIRAMBI
Zilisomwa rambirambi zilizotumwa kwa mkuu wa
majeshi kutoka sehemu mbalimbali, zikiwamo toka kwa mabalozi, maofisa wastaafu,
wanajeshi wenzao walio Unamid-Sudan na Jumuiya wa Watanzania wanaoishi Sudan.
Aidha, Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Sudan walitoa Dola za Marekani 700
kama rambirambi na wanajeshi wenzao walitoa Dola 1,800 kwa marehemu
wote.
UN YATOA
NISHANI
Katika kutambua mchango wa wanajeshi hao, UN
ilitoa medali kwa kila mwanajeshi aliyefariki ambazo kwa mujibu wa Msemaji wa
shughuli hiyo ya jana, Kanali Dominick Mrope, zitafikishwa kwa wanaostahili, kwa
mujibu wa taratibu za kijeshi.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ),
Dk. Ali Mohamed Shein, alituma rambirambi kwa mkuu wa majeshi na katika salamu
zake zilizosomwa kwa niaba yake na Kamanda wa Kamandi ya Nchi Kavu, Meja
Jenerali Mustapha Kijuu, alisikitikia mauaji yaliyofanywa dhidi ya mashujaa
hao.
“Natoa salamu zangu kwako mkuu wa majeshi na
kwa familia za wafiwa, kufuatia msiba huu mkubwa wa kitaifa. Naomba tuwe na
subira na nawatakia nafuu ya haraka, majeruhi wote walioko hospitalini,”
alisema.
JK ANENA
Kwa upande wake, Rais Kikwete alisema kwamba
atahakikisha anatumia ushawishi wake wote ili kuzishawishi mamlaka za UN na
Umoja wa Afrika (AU) zinazosimamia operesheni za amani Darfur, ili ziweze
kuruhusu vikosi vinavyoshiriki katika operesheni hizo, kuwa na silaha nzito kwa
minajili ya kujilinda kwa mapigo mazito, pale zinaposhambuliwa.
“Nilisikitika sana pale nilipopata habari ya
kuuawa kwa mashujaa wetu. Nilijiuliza kwamba, kwa nini watu wa Darfur wawaue
wanajeshi wetu walioenda kuwasaidia wapate amani, waendeshe maisha yao katika
hali ya utulivu. Ndiyo maana niliongea na Rais Omar al Bashir, ahakikishe
wanawatafuta wahalifu hawa haraka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria,”
alisema.
Hata hivyo, Rais aliwaasa Watanzania na
wanajeshi kwa ujumla kutokatishwa tamaa na kilichotokea, bali wachukue kama
changamoto ya kujiimarisha zaidi.
Aliwakumbusha Watanzania kuwa toka uhuru,
Tanzania imekuwa na falsafa ya kusaidia mataifa mbalimbali kwa njia za
kidplomasia na kivita, ili yapate amani kama ilivyofanyilka katika nchi za
Msumbiji, Liberia, Sierra Leone, Eritrea, Lebanon, Sudan na sasa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo.
Alisema tokea Tanzania ianze kuchangia
wanajeshi wake kule Sudan, mwaka 2007, JWTZ imefanya kazi zake kwa weledi na
umakini wa hali ya juu, kiasi
0 comments: