SAMATTA, ULIMWENGU WATUA ACCRA GHANA KUJIWINDA DHIDI YA SETIF


Samatta (kushoto) akiwa na Ulimwengu (kulia) na Sure Boy katika kikosi cha Taifa Stars
Washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wako nchini Ghana kujiandaa na mechi za robo fainali ya Kombe la Shirikisho.
Samatta na Ulimwengu wako mjini Accra na kikosi cha TP Mazembe ambako watakuwa wakifanya mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Setif na Watanzania hao wanaonekana kuwa tegemeo la ushambuliaji kwa kushirikiana na Tresor Mputu na Mzambia, Given Singuluma.
Katika kikosi hicho kilichoondoka mjini Lubumbashi, juzi na kutua Kinshasa kwa muda kabla ya kumaliza safari yake jijini Accra, kocha wa Mazembe aliamua kumuacha

0 comments:

ZIARA YA OBAMA YAFUNIKWA NA MANDELA, WATUWENGI HAWAKUMLAKI BADALA YAKE WAMEJAZANA HOSPITALINI KWA MANDELA

.
ANGALIA PICHA....OBAMA NA MKEWE WAKIWA WAMEVAA VAZI LA KIASILI LA KIZULU 
Ziara ya Rais wa Marekani Obama imeingia doa nchini Afrika kusini baada ya watu wengi kutirilika Hospitalini alipolazwa mzee Mandela badala ya kwenda uwanja wa ndege kumlaki Rais huyo amabae hujio wake umekuwa na na maandalizi makubwa Barani Afrika ambako amepanga kutembelea nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania

0 comments:

MASWAHIBA WA PELE NA AZAM AKADEMI SASA WAENDA KUTETEA TAJI LAO MKOANI ARUSHA WAKIWA KAMILI

Maswahiba wa Pele; Azam Akademi wakiwa na Pele alipowatembelea Chamazi mwaka jana

MABINGWA watetezi wa Kombe la Rollingstone, michuano ya kila mwaka mjini Arusha, Azam Akademi wanatarajiwa kuondoka wiki ijayo kwenda mjini humo tayari kutetea taji lao.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga  jana  amesema kwamba, Akademi wamekuwa kwenye mazoezi makali chini ya makocha wao, Vivek Nagul, Iddi Cheche na Philipo Alando kujiandaa na michuano hiyo.
Amesema maandalizi ya vijana yamekuwa ya muda mrefu na sasa wako fiti kwenda kuendeleza utemi wao katika michuano hiyo maarufu

0 comments:

LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMZIE MAMBO YA USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA AKIWA TANZANIA



Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
 
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ameliambia NIPASHE Jumapili ofisini kwake jijini hapa jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.
Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
 
“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.
Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
 
"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.
Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia

0 comments:

DONGO LA SUMAYE KUHUSU AJIRA KWA VIJANA LAMKOROGA EDWARD LOWASSA

WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya tatu, Frederick Sumaye, amesema kuwa katu kukosekana kwa ajira nchini kwa vijana si bomu linalosubiri kulipuka. Bila kumtaja jina kauli hiyo ya Sumaye ilionekana kumlenga Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye hata hivyo bomu alilokuwa akilizungumzia ni ajira. Jana akizungumza na vijana wa Kawe Jogging, Sumaye alisema kauli kama hiyo imekuwa ikiwafanya vijana wajione ni kundi lingine, huku akihoji hatua walizochukua watu

0 comments:

SIRI YA ZIARA YA OBAMA SASA YAJULIKANA SHUGHULI NZIMA YA MAANDARIZI YAKE KUFANYWA NA MAAFISA WA MAREKANI





 MAANDALIZI ya ziara ya Rais wa Marekani hapa nchini, Barack Obama yamezidi kushamiri na sasa Wamarekani ndio wanaoongoza karibu kila idara wakitumia vifaa vyaoEneo ambalo linaonekana kumilikiwa na Wamarekani kwa asilimia karibu zote ni lile la mawasiliano, ambapo inaelezwa kuwa maofisa wao ndio watakaoongoza kila kitu ikiwemo kufanya ukaguzi wa watu watakaoingia uwanjani hapo kesho kwa ajili ya kumlaki Obama. Habari

0 comments:

OBAMA AFUTA ZIARA ZAKE ZA KUTEMBELEA MBUGA ZA WANYA YADAIWA NI KUTOKANA NA VURUGU ZA KISIASA ZILIZOTOKEA MKOANI ARUSHA NDIO ZIMESABABISHA


MADHARA ya vurugu za kisiasa mkoani Arusha zinazodaiwa kusababishwa na polisi kukabiliana na wafuasi wa vyama vya upinzani, zimesababisha pigo kubwa kiuchumi katika ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Pigo hilo ambalo limesababisha serikali na mahoteli ya kitalii mkoani humo kukosa mabilioni ya fedha, limetokana na hatua ya rais huyo na ujumbe wake kufuta ziara yake kwenye mbunga za wanyama za Serengeti na Mikumi.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni pigo kwa serikali ambayo ilitarajia kuingiza mabilioni ya fedha baada ya rais huyo maarufu duniani na ujumbe wake wa watu 700, kuzuru kwenye hifadhi hizo za taifa.
Rais Obama ambaye alianza ziara yake barani Afrika nchini

0 comments:

KIKWETE AMCHENJIA WARIOBA KWAKURIDHIA MABADIRIKO YA KATIBA KUTAKA UWEPO MUUNDO WA SERIKALI MBILI

 
RAIS Jakaya Kikwete amemgeuka Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kwa kuridhia azimio la Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutaka uwepo muundo wa serikali mbili.
Rais Kikwete ambaye juzi aliongoza kikao cha Kamati Kuu (CC), mjini Dodoma, aliridhia azimio hilo, huku akijua fika kuwa ndiye aliyemruhusu Jaji Warioba kuingiza kipengele hicho kwenye rasimu wakati alipoifikisha mbele yake kabla ya kuitoa hadharani.
Kutoka na hali hiyo, Kamati Kuu imewataka wanachama wao wote kupitia mabaraza ya CCM kuhakikisha wanakubaliana na msimamo wa chama wa kupinga muundo wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa

0 comments:

BREAKING NEWS KIONGOZI WA CCM GAIRO MKOANI MOROGORO AMWAGIWA TINDIKALI



Meza yetu ya habari imepokea taarifa toka Gairo - Morogoro kuhusiana na tukio la  kumwagiwa kwa tindikali Mwenyekiti wa CCM mjini hapo.  Inasemekana watu wasiojulikana jana usiku walimmwagia tindikali Mwenyekiti wa CCM Gairo  akiwa maeneo ya

0 comments:

PINDA ATILIA MSISITIZO KAULI YAKE SASA HASEMA ASEMA NJIA YA KUEPUKANA NA VURUGU NI KUTOWAONEA HURUMA WANANCHI WANAO LETA FUJO

Serikali imesisitiza kuwa haitavumilia kuona baadhi ya watu wanaendelea kupanda mbegu za chuki za kidini na kisiasa miongoni mwa Watanzania na imesisitiza kuchukua hatua bila huruma kuzimaliza njama hizo. Kauli hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana, wakati akiahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge hadi Agosti 27, mwaka huu.
“Nataka niwahakikishie Watanzania kuwa serikali haitavumilia hata kidogo kuendelea kupandwa mbegu za chuki na za kidini na kisiasa miongoni mwa Watanzania.
“Serikali itachukua hatua kali bila huruma kuzima njama hizi mbaya dhidi ya taifa letu…vile vile, hatua kali zitachukuliwa kwa mtu yeyote ataka

0 comments:

ROMBO KIMENUKA POLISI WAAMUA KUSIMAMIA MAZISHI BAADA YA VURUGU KUTOKEA MSIBANI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema
KATIKA hali isiyo ya kawaida Jeshi la Polisi wilayani Rombo,limelazimika kusimamia shughuli ya mazishi baada ya kundi la watu wanne kuzuia mwili wa marehemu Gaspar Evarist (18) aliyefariki kwa ajali ya pikipiki usizikwe shambani kwake kijiji cha Muriae, wilayani Rombo.
Mkuu wa Polisi wilayani hapa, Ralph Meela alisema kuwa vurugu hizo zilisababishwa na mama wa marehemu huyo na watoto wake wakitaka mwili huo usizikwe kwenye shamba la baba yake mzazi bali wakauzike sehemu nyingine.
Akifafanua zaidi Meela alisema chanzo cha mzozo huo ni baba wa marehemu kufariki miaka mingi iliyopita na hivyo waliokuwa wakizuia mwili huo walidhani kuwa endapo marehemu atazikwa hapo shamba hilo litakua la kwake na hivyo watakosa urithi.
Alisema katika vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa mali, kwani wahusika walivunja msalaba wa jumuiya pamoja na kumzuia padre kuendesha ibada ambaye ndugu walimtishia na hivyo kuondoka kuepuka vurugu hizo.
Baada ya polisi kufika waliwakamata watuhumiwa na kisha kusimamia mazishi hayo.
Wakati huo huo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la

0 comments:

EXCLUSIVE: JUMA KASEJA AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUTEMWA NA SIMBA - HAJAPEWA TAARIFA RASMI NA SIMBA....


Juma Kaseja akijifua na vijana wadogo mkoani Kigoma wanaotaka kufuata nyayo zake.
Siku moja baada ya klabu ya Simba kupitia mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope kuthibitisha kwamba golikipa mkongwe wa timu hiyo Juma Kaseja hatoongezewa mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo aliyoichezea kwa takribani miaka 10, leo hii mtandao huu umepata nafasi ya kuongea na Juma Kaseja kutaka kujua anazungumziaje uamuzi huo wa Simba.
Kaseja ambaye ni golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania kwa sasa yupo kwao mjini Kigoma alipoenda kupumzika baada ya

0 comments:

MSANI WA FILAMU NA NYIMBO ZA KIZAZI KIPYA MAARUFU KAMA BABAY MADAHA ALIZWA NGUO ZAKE ZA NDANI

KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu na muziki Baby Joseph Madaha amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuibiwa nguo zake za ndani alizokuwa ameanika nje maeneo ya Mikocheni jijini Dar.
Chanzo  cha habari ambacho ni shosti wa karibu wa mwanadada huyo kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitiririka:
“Alizifua kama dazeni nzima hivi na kuzianika nje kisha kwenda kwenye mishe zake. Heh! Kumbe vibaka hawaachi kitu, waliruka fensi wakazi

0 comments:

CHADEMA WAAMUA KUMFUNGUKIA WAZIRI MKUU SASA WAAMUA KUMJIBU LAIVU LAIVU BILA CHENGA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema kimeibuka jana bungeni na kusema Serikali inafahamu ukweli wa mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa chama hicho jijini Arusha.Chama hicho kimesema Serikali ilitumia kutokuwepo kwao bungeni kupotosha wananchi kuhusu hali halisi juu ya mlipuko wa bomu hilo uliotokea wakati chama hicho kikihitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Viwanja vya

0 comments:

MFALME MASWATI III NAE AINGIA TANZANIA KUSHIRIKI KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA SMART PERTINER SHIP



Mfalme Mswati III akiwa sambamba na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal sambamba na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mfalme Mswati II wa Swizland baada ya kuwasili nchini jana kuhudhuria mkutano wa ‘Smat Patnership’, unaotarajia kuanza kesho. Kushoto ni Mke wa Mfalme huyo.

Wasaidizi wa Mfalme Mswati wakimsubiri Mfalme huyo baada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania

0 comments:

HOSPITALI ALIYOLAZWA MANDELA KWAWAKA MOTO MAMIA YA WATU WATIRIRIKA KUMTAKIA HERI

Mamia ya watu wanaendelea kukusanyika nje ya hospitali alikolazwa Nelson Mandela mjini Pretoria Afrika Kusini. Inaarifiwa Mandela bado yuko hali mahututi. Wamekuwa wakimuimbia nyimbo na kumuombea nje ya hospitali. Wengine wamekusanyika katika iliyokuwa makaazi ya Mandela mtaani Soweto. Watu wana wasiwasi kuhusu hali y mandela lakini pia wanataka kuonyesha wanavyojivunia kiongozi wao ambaye

0 comments:

KAMPENI ZA WINDA ZATANGAZA MSHINDI WA DROO HIYO NI MWALIMU WA TABATA SHULE YA SEKONDARI TABATA

Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo (wa pili kulia) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde Mwl.Michael Valerian Mbuya katika mkutano na wana habari uliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Meneja mauzo wa Push Mobile Rugambo Rodney, kulia kwake ni Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko na Mkaguzi

0 comments:

HAWA NDIO MABINGWA WA RISING AIRTEL STARS KINONDONI,MAKUMBUSHO UNITED

Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akipokea kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kutoka kwa Ofisa Maendeleo wa TFF Bw. Salum Madadi baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika mchezo wa mwisho wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 uliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013.
 

Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akinyanua juu kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika fainali ya mashindano hayo ngazi ya mkoa iliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013.

Wachezaji wa timu ya Makumbusho United wakishangilia baada ya kutwaa kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013. Makumbusho walishinda 5-1 dhidi ya Mtakuja.
 

Baadhi ya mashabiki wa kishangilia timu zao katika michuano ya Mkoa ya Airtel Rising star 2013
Timu ya Makumbusho United imetawazwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni baada ya kuwafunga bila huruma Mtakuja Beach 5-1 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ya vijana chini ya umri wa miaka 17. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha shule ya Msingi Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo Juni 25 ,2013.
Mabingwa hao wapya wa ARS ngazi ya mkoa walianza

0 comments:

EOTF WANAWAKE WAKIWEZESHWA KIUCHUMI NA WAKIPEWA ELIMU YA UJASILIAMALI WANAWEZA KUTOKOMEZA UMASIKINI

Mama Anna Mkapa akizungumza katika semina hiyo
Washiriki mbalimbali katika semina hiyo
Picha ya pamoja kati ya Washiriki mbalimbali katika semina hiyo na mgeni rasmi.
WANAWAKE wakiwezeshwa kiuchumi na ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu ya ujasiriamali, kuepuka maradhi hatarishi na kufahamu haki zao katika jamii hali ya umaskini itapungua kwa kile kipato kuongezeka katika kundi hili kubwa la Watanzania.
Kauli hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya wanawake wajasiriamali yanayoendelea kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani.
Mama Anna Mkapa ambaye pia ni Mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii wajasiriamali hao kutoka

0 comments:

OMMY DIMPOZ APATA SHAVU LA KUFANYA TOUR MAREKANI NA CANADA

Omary Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya DMK Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kumaliza tour nyingine barani ulaya.

"Yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri

0 comments:

''MSIJE DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA KWANI HUDUMA NYINGI ZA KIJAMII ZITAKUA NISHIDA''NI KAULI YA MEMBE ALIPOKUA AKITOA RIPOTI HIYO CLOUDS RADIO


Dar es salaamWaziri wa mambo ya njee Benard Membe amewashauri watu kusitisha safari zao za kuja jijini humo kutokana na ujio wa Rais wa marekaani Barack Obama anyetarajia kuwasili nchini na akiwa na wageni wengi.Ugeni huo ni pamoja na hule wa wageni kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani wanaotarajia kuudhiria mkutano wakimataifa SMART PARTINERSHIP utakaofunguliwa na Rais Kikwete kwenye ukumbi wa mikutano wakimataifa wa Julius Nyerer.Ulinzi umeimarishwa

0 comments:

KITUO CHA HAKI ZA BINADAMU CHAMKALIA KOONI WAZIRI PINDA CHAMTAKA AFUTE KAULI YAKE YA ''WAPIGWE TU ''ALIOITOA BUNGENI

Waziri mkuu Mizengo Pinda

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha haki za binadamu (Legal and Human Right Center) Daktari Helen Kijo-Besimba (kulia )
Taarijfa hii ni matokeo ya ufuatiriaji utendaji wa shughuli za serikali kama zinavyowasilishwa Bungeni na kauli ya Waziri mkuu Mizengo Pinda alietoa kauli hiyo Bungeni siku ya tarehe juni 20 2013 wakati akijibu maswali y a papo kwa hapo.Waziri Mkuu Pinda alivitaka vyombo vya Ulinzi na

0 comments:

BRAZIL YAIFUNGA URUGUAY MABAO MAWILI KWA MOJA KATIKA MICHUANA YA NUSUFAINALI KOMBE LA MABARA


Hili ndilo goli lililowasambaratisha Urugauy katika michuano ya kombe la mabara

.

0 comments:

RATIBA YA ZIARA YA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA YATOKA, ATAKAA SIKU MBILI TU


 
Rais Barrack Obama
Ikulu ya Marekani na Idara ya Habari (Maelezo), wametangaza ratiba ya Rais Barrack Obama atakapozuru Tanzania huku ikionyesha kuwa atakaa siku mbili tu, kuanzia Julai Mosi na kuondoka kesho yake.
 
Tanzania itakuwa nchi ya mwisho ya Afrika kutembelewa na Obama baada ya Senegal na Afrika Kusini. Mara atakapowasili na ndege yake kubwa ya Air Force One, Rais Obama atazindua barabara mpya katika

0 comments:

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNE 27 2013

DSC 0046 4407f

DSC 0047 e9908
DSC 0048 11dd9
DSC 0049 1485b
DSC 0050 83fa3
DSC 0051 84657
DSC 0052 e450a
DSC 0053 5db36
DSC 0054 a51b5
DSC 0055 86fa5
DSC 0056 dbf87
DSC 0057 c31ab
DSC 0058 bd1e6
DSC 0059 e66c8

0 comments:

UMEISOMA HII MWADADA AMZAWADIA CHRIS BROWN MAARUFU KAMA ''BREEZY'' CHUPI YAKE

Huyu ndiye Carol aliyempa Breezy nguo yake ya ndani
Mastaa ni watu ambao hukutana na mambo mengi sana yakiwemo ya kushangaza kutokana na kwamba tayari wao ni maarufu na watu wengi wa kawaida hutamani hata ule ukaribu nao tu ili, kuzifurahisha nafsi zao. Mwimbaji wa R & B Chris Brown weekend iliyopita amekutana na mtego wa aina yake kutoka kwa msichana ambaye inaonekana alimtamani.
Wakati Chris Brown yuko jukwaani anatumbuiza katika show ya Anaheim Jumamosi usiku (June 22), shangwe za kutosha zilisikika

0 comments:

ZANTEL SASA YAZINDUA HUDUMA YA DAKTARI KWENYE SIMU YA MKONONI

Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali Watu cha Zantel, Francis Kiaga akifafanua jambo wakati wa ushirikiano na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa na lengo la kupata ushauri kwa masaa 24 mahali popote nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa BR Solutions, Richard Toba na Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan. (Picha na Habari Mseto Blog)
Mkurugenzi Mkuu wa BR Solutions, Richard Toba (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Dk. Aidan Njau akifafanua jambo, Sajid Khan. 

DAR ES SALAAM, Tanzania

KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Zantel imezindua ushirikiano na Kampuni ya BR Solution na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuwawezesha watanzania kupata huduma ya ‘Daktari kwa njia ya simu’ ikiwa ni kupata ushauri kwa masaa 24 mahali popote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Zantel jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel Francis Kiaga alisema, wameamua kuingia ubia na Wizara pamoja

0 comments: