AU KUJADILI HOJA YA KUJIONDOA ICC

 
Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kukutana mwezi ujao mjini Addis Ababa Ethiopia, kujadili msimamo wa bara hili kuhusu iwapo watajiunga na Kenya katika kujiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifiu - ICC.
Mkutano huo unafuatia ombi la Kenya kutaka kikao cha dharura cha Umoja wa Afrika kujadili kesi zinazowakabili Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.
Mwandishi wa BBC mjini Addis Aabab, Emmanuel Igunza anasema kuna dalili kuwa ombi hilo la Kenya limeanza kuungwa mkono na mataifa mengi barani.
Kwa sasa hakuna dalili kuwa kuna msimamo mmoja kuhusu ikiwa wanachama 54 wa Muungano wa Afrika waliotia saini mkataba wa Roma wanataka kujiondoa, lakini marais wa nchi hizo bado watajadili uwezekano wa wanachama 34 wa mkataba wa Roma uliounda mahakama ya ICC watajiondoa ICC.
Tangu kuanza kwa kesi ya Naibu rais wa Kenya William Ruto katika mahakama ya ICC wiki jana, na ile ya Rais Kenyatta ikitarajiwa kuanza mwezi Novemba, dalili zimeonekana kuwa wengi hawana imani na mahakama hiyo wakiiona kama chombo cha nchi za Magharibi kukandamiza waafrika.
Kikao cha dharura sasa kimepangwa kujadili swala hilo baada ya Kenya kuonekana kutaka kuungwa mkono katika azma yake ya kujiondoa ICC.
Kuna uwezekano wa nchi wanacahama wa mkataba wa Roma kujiondoa ICC lakini bado kuna nafasi ya maombi mengine kufanywa kuhusiana na hilo.
Share on Google Plus

0 comments: