RAIS OBAMA AMPONGEZA MWANAUME SHOGA ALIYEJITANGAZA HADHARANI


Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini Marekani mwenye asili ya Afrika 
Jason Collins amejitangaza kuwa yeye ni shoga hatua ambayo 
imewashitua watu wengi hususani wapenzi wa mchezo huo. 
Jason Collins anakua mchezaji wa kwanza wa kimataifa mwanaume 
ambaye bado anacheza mpira wa kikapu kutangaza kuwa ni shoga huku akisema kuwa yeye ni mwanamme mweusi na ni shoga. Rais wa Marekani Barack Obama amempongeza mwanababa huyo shoga mwenye umri wa......
miaka 34 anayecheza katika ligi ya NBA kwa kujitangaza hadharani. Rais Obama ambaye mwaka jana alitangaza kuunga mkono ndoa za mashoga alimpigia simu Collins na kumpongeza kwa ujasiri alioonyesha.
Share on Google Plus

0 comments: